Video Vixen Kidoa Amkingia Kifua Hamisa Mobetto.....Adai Wasanii Wenzake Wanamyanyapaa


MUUZA nyago matata Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’, amewataka mastaa wa kike Bongo waache kuendelea kumuandama mwanamitindo, Hamisa Mobeto baada ya kuzaa na Mbongo Fleva ambaye ni mzazi mwenza wa mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, kwani jambo hilo linamuathiri kisaikolojia.


Akibonga na Star Mix, Kidoa ambaye anashikilia Taji la Ijumaa Sexiest Girl 2015 alisema kuwa, jambo ambalo linamstajabisha ni kitendo cha mastaa wengi Bongo kumsapoti Zari na kumponda Hamisa, kana kwamba hawamjui ilihali ni Mbongo mwenzao.

“Siyo sawa wasanii wenzangu wanavyomnyanyapaa Hamisa, kutwa kumpiga vijembe, wanapaswa kukumbuka kuwa hakuna ajuae kesho yake, huenda hata yeye hakuwaza kama yangemfika hayo,” alisema Kidoa 
Video Vixen Kidoa Amkingia Kifua Hamisa Mobetto.....Adai Wasanii Wenzake Wanamyanyapaa Video Vixen Kidoa Amkingia Kifua Hamisa Mobetto.....Adai Wasanii Wenzake Wanamyanyapaa Reviewed by Admin on Monday, November 13, 2017 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.