Mahakama Kuu yatengua kufukuzwa kwa wabunge 8 wa CUF

Mahakama Kuu Ijumaa hii imetengua kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananchi, CUF na kusitisha pia mchakato wa kuwafukuza uanachama mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.


Prof Ibrahim Lipumba
Aidha Mahakama hiyo pia imemzuia Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF kujadili kuhusu uanachama wa Wabunge na Madiwani hao.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma ya CUF Taifa, imeeleza kuwa, Mahakama Kuu imekubaliana na Hoja za Wabunge 8 wa chama hicho na imeona hoja za msingi za madai yao zinazopaswa kuangaliwa kuhusu uhalali wa masuala yote yaliyowasilishwa mbele ya Mahakama hiyo.
Imefafanua kwamba, Mahakama Kuu pia imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliyowekwa na Prof. Lipumba na Wenzake katika shauri hilo.
Mahakama Kuu yatengua kufukuzwa kwa wabunge 8 wa CUF Mahakama Kuu yatengua kufukuzwa kwa wabunge 8 wa CUF Reviewed by Admin on Saturday, November 11, 2017 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.