Fiston Kayembe
Huyu ni mchezaji anayecheza kama beki wa kati na tayari kuna taarifa kuwa Mwalimu George Lwandamina amevutiwa na uwezo wake katika nafasi hiyo, Huyu unaweza ukahisi kama hana nafasi katika kikosi cha Yanga lakini Yanga hawajiandai katika michezo ya Ligi pekee bali hata katika michuano ya KIMATAIFA ambapo Yanga ndiyo mwakilishi wa klabu bingwa Afrika.
Mohammed Rashid
Kutokana na kuwa na majeruhi katika safu yake ya Ushambuliaji na kutokuwa na Uhakika kama majeruhi hao watapona kwa wakati basi msomaji wa Kwataunit.com unaambiwa Klabu ya Yanga wanafanya juu chini kuhakikisha Mshambuliaji wa Tanzania Prisons Mohammed Rashid Anatua Yanga.
Mohammed Rashid ameanza vyema msimu huu akipachika mabao 6 katika mechi 9 alizocheza huku vilabu vingi vikubwa vikitoka udenda kuwania Saini Yake.
Mohammed Ibrahim "Mo"
Huyu ameonekana kutokuwa na Furaha katika klabu yake ya Simba na hii ni kutokana na kukosa namba ya Uhakika baadhi ya washabiki wa klabu ya Simba wamekuwa wakimlaumu kocha Omog kwa kutomtumia wakiamini ni mzuri na anafaa kucheza.
Yanga msomaji wa Kwataunit.com wamekuwa wakitajwa kumnyemelea ili kuzidi kujiimarisha hasa maeneo ya Pembeni (Wings) na Hii inatokana na klabu hiyo kupunguza Nguvu yake katika maeneo ya Pembeni. Lakini inaweza ikawa ngumu kwa mchezaji huyu kutua Yanga hasa kutokana na ukweli kwamba Yanga na Simba huwa ni Ngumu kuuziana wachezaji hasa kama bado wanamikataba na timu zao.
Mohammed Issa " Banka"
Banka moja kati ya Viungo washambuliaji bora kwasasa nchini akiwa kaonyesha uwezo wa hali ya juu kiasi cha Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara Salum Mayanga Kumuita Timu ya Taifa, Huyu anatajwa kutua Yanga kusaidiana na Kina Tshishimbi eneo la Kati hii ni kutokana na Kamusoko kuwa na majeruhi ambayo hayaeleweki kama atapona mazima. Kuzipa tetesi za Usajili kila siku like Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini.
USAJILI DIRISHA DOGO, HAWA WANAWEZA WAKATUA YANGA
Reviewed by Admin
on
Friday, November 17, 2017
Rating:
No comments:
DONDOSHA COMENT YAKO HAPA