Afisa habari makini Dismas Ten ambaye ndiye mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano katika klabu ya Yanga amesema wao kama uongozi wa Yanga hawajatoa taarifa yoyote na hawajazungumza na Singida United.
''Huwezi kuwazungumzia watu kuzungumza lakini sisi kama klabu hatujatoa taarifa kuhusiana na jambo hilo na hakuna mazungumzo yoyote na Singida United kuhusiana na suala hilo. ,,
Kuhusu kama Yanga wako tayari kufanya ubadilishano huo Dismas Ten amesema
'' Hilo ni suala la Upande mwingine, siyo suala geni kwenye mpira wa Miguu mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine ni suala ambalo lipo toka mpira wa miguu umeanzishwa kikubwa ni kufuata utaratibu na kuangalia maslahi ya pande zote klabu na wachezaji husika kwahiyo suala linajadiliwa kwa taratibu husika.,,
Ukweli Kuhusu DONALD NGOMA Kwenda Singida United? Huu Hapa
Reviewed by Admin
on
Wednesday, November 15, 2017
Rating:
No comments:
DONDOSHA COMENT YAKO HAPA