Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeanika mali za aliyekuwa Mhasibu Mkuu wake, Godfrey Gugai, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa wa thamani ya Sh. bilioni 3.5.
Mhasibu huyo anatuhumiwa kujipatia mali nyingi kinyume na sheria ambapo miongoni mwa mali zilizotajwa kwamba anazimiliki ni pamoja na viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki.
Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo ambaye alishafukuzwa kazi tangu mwaka jana viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi na Kiseke jijini Mwanza.
Mali hizo kwa sasa zinashikiliwa na TAKUKURU kutokana na kibali ilichopewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupeleka maombi ya kuzikamata.
Mei 8, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ya zuio la mali za Gugai ambaye anakabiliwa na tuhuma za kujilimbikizia mali kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
Amri ya zuio la mali za Gugai ilitolewa na Mahakama hiyo kutokana na ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) chini ya kifungu namba 38(1)(a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 katika shauri namba 13 la 2017.
Mali zilizozuiwa na mahakama ni;
Nyumba nne za ghorofa moja moja zilizoko kiwanja na 64 kitalu Ununio, Kinondoni,
Nyumba tatu za ghorofa moja zilizoko kiwanja na 150 kitalu 8 Bunju na Kinondoni,
Nyumba nne zilizoko Kiwanja na 225 Kitalu 6, Mbweni JKT, Kinondoni.
Nyumba zilizoko kwenye kiwanja namba 62 na 63 kitalu C, Kinondoni,
Nyumba iliyoko kiwanja namba 29 kitalu L, Majita, Musoma,
Nyumba namba 713 PPF Kiseke, Mwanza na
Nyumba iliyoko kwenye kiwaja namba 438 bloku D, Nyegezi, Mwanza.
Kiwanja namba 14 kitalu J, Bunju, Kinondoni,
Kiwanja namba 47 kitalu B, Mwongozo, Kigamboni,
Kiwanja namba 184 kitalu B, Buyuni,Temeke,
Kiwanja namba 103 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo,
Kiwanja namba 104 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo na
Kiwanja namba 209 kitalu B, Kibaha.
Kiwanja namba 195 kitalu 3, Kihonda, Morogoro,
Kiwanja namba 993 kitalu L, Kiegeya, Morogoro,
Kiwanja namba 868 Kitalu Q, Lukobe, Morogoro,
Kiwanja namba 34 kitalu K, Kisasa B, Dodoma,
Kiwanja namba 32 kitalu N, Itega, Dodoma,
Kiwanja namba 39 Kitalu M, Itega, Dodoma,
Kiwanja namba 24 kitalu B, Chidachi, Dodoma,
Kiwanja namba 64 Nzuguni, Dodoma,
Kiwanja namba 230 Kitalu B, Nyegezi, Mwanza na
Kiwanja namba 439 Kitalu D, Nyegezi, Mwanza
Kiwanja namba 275 Kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza,
Kiwanja namba 277 kitalu 2 Nyamhongolo, Mwanza,
Kiwanja namba 296 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza,
Kiwanja namba 297 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza,
Kiwanja namba 286 kitalu G, Nyamagana, Mwanza,
Kiwanja namba 287 kitalu G, Nyamagana, Mwanza,
Kiwanja namba 90 kitalu 5, Bugarika, Mwanza,
Kiwanja namba 126 kitalu A, Makoko, Musoma,
Kiwanja namba 622 kitalu A, Gomba , Arusha,
Kiwanja namba 621 na 623, kitalu A, Gomba na Arusha,
Kiwanja namba 737 kitalu C, Mwambani, Tanga
Kiwanja namba 1,2 na 3 kitalu J, Mwambani,Tanga,
kiwanja namba 4 kitalu J Mwambani, Tanga,
Kiwanja namba 5 kitalu J, Mwambani Tanga,
Kiwanja namba 18 kitalu J, Mwambani Tanga,
Kiwanja namba 7,9 kitalu J, Mwakidila, Tanga na
Kiwanja namba 11, 13 kitalu J, Mwakidila, Tanga
Gari namba T 180 DBQ , Mitsubish Canter,
Gari namba T 581 BQU, Toyota Hillux,
Gari namba T 814 CSC Nissan Murrano,
Gari namba T 679 ASD Toyota RAV 4 na
Gari namba T 913 DHE Suzuki
Pikipiki yenye namba ZZ usajili MC 837BCL
Kutokana na maombi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) mahakama imeamuru mali zilizotajwa hapo juu chini ya zuio la Mahakama. Aidha, mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.
Pia, Msajili wa hati ameagizwa kusajili zuio hilo kama kizuizi dhidi ya mali zote zilizotajwa.
Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza vinginevyo.
Hivi karibuni Gungai anafikishwa mahakamani akikabiliwa na mshtaka ya rushwa na mengine yanayofanana na hayo.
Orodha ya Mali za Mhasibu wa Takururu Godfrey Gugai Zinazoshikiliwa na Mahakama ni Kufuru
Reviewed by Admin
on
Wednesday, November 15, 2017
Rating:
No comments:
DONDOSHA COMENT YAKO HAPA