Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameeleza hisia zake kwa kile ambacho anapitia kwa sasa katika maisha yake.
Mrembo hiyo amesema licha ya magumu anayokabiliana nayo kwa sasa bado anaamini Mwenyenzi Mungu atamvusha. Kupitia mtandao wa snapchart ameandika;
Bado sijafika Mw/Mungu aliponipangia na kama mnavyoona barabara yangu ni mbovu, ina mashimo, mabonde na pia matope mengi kwa hiyo safari yangu inakuwa ngumu kidogo.Lakini naimani sana na M/Mungu alonileta kwenye dunia hii, naimani ipo siku nitafika na Naimani barabara yangu hii nii mbovu ipo siku ataisawazisha na kuiweka rasmi.Nina kushukuru sana Mungu, naimani kuna vibaya vingi umeniepusha navyo na pia naimani kuna vikubwa vizuri vyaja. Na naimani hivi vyote visingenipata mimi kama ningekuwa sina u-special wowote ndani yangu.
Hamisa ambaye amezaa na Diamond Platnumz mtoto mmoja aliwahi kuingia katika mvutano na Zari The Boss Lady ambaye alikuwa mpenzi wa muimbaji huyo. Hivi karibuni Hamisa amekuwa akihusishwa katika drama la Diamond kurudiana na Zari mara baada ya kudaiwa walikuwa pamoja hivi karibuni.
''Kama mnavyoona barabara yangu ni mbovu'' Hamisa Mobetto
Reviewed by Admin
on
Tuesday, June 05, 2018
Rating:
No comments:
DONDOSHA COMENT YAKO HAPA