BEEF ALERT : Ni Vigumu Msanii Kushindana na Producer - Mr T Touch


Producer kutoka Touch Sound, Mr. T Touch amesema ni vigumu kwa msanii kushindana na producer.

Kutokana na hilo Mr. T Touch amesema hawezi kushindana vita ambayo anajua atashinda.

“Wale ni wasanii wanaenda wanaonekana mbele ya macho ya watu wengi kuliko sisi ma-producer, watu wengine wameanza kuona sura ya T Touch hivi karibuni lakini kila kitu kinaenda kwa wakati,” amesema.

“Lakini ukisema kwamba tushindane, msanii hawezi kushindana na producer, mimi naweza kutoa ngoma za wasanii watatu kwa mpigo na zika-hit zote lakini msanii unapotoa wimbo unategemea utashindana na producer,” Touch ameiambia Bongo5.

Kauli ya Mr. T Touch inakuja mara baada kumchukua aliyekuwa msanii wa Nay wa Mitego, B Gway kutoka Free Nation ambapo awali alikuwa akifanya kazi Mr. T Touch. B Gway anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Na Stay. 

BEEF ALERT : Ni Vigumu Msanii Kushindana na Producer - Mr T Touch BEEF ALERT : Ni Vigumu Msanii Kushindana na Producer - Mr T Touch Reviewed by Admin on Tuesday, June 05, 2018 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.