Msanii wa Filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka ukaribu wake na Alikiba.
Wolper amelazimika kuzungumzia ukaribu wake na msanii huyo mara baada ya kuandika ujumbe wenye hisia za aina yake katika kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Alikiba.
“Hatuna urafiki lakini ni mtu ambaye namjua toka zamani kabla ya yeye hajawa staa na mimi sijawa staa, kwa hiyo tunajuana zamani lakini pia hatujawahi kukoseana adabu, kutukanani kwenye mitandao au kukosoana” Wolper ameiambia FNL ya EATV.
“Kuna vitu ambavyo ameniheshimu, unapomu-wish mtu kuna feeling, kile kitu ambacho kinakujia moyoni inabidi ukifanye na kimeshakujia, so ilinijia na kuna vitu nilikumbuka nikasema ngoja niandike kwa sababu ni kweli kutokana na tulivyokuwa tunaishi miaka ya 2000 huko” amesisitiza.
Ujumbe alioandika Wolper kwa Alikiba ulisomeka, “Happy birthday to you Ally!I love you and you know that!More life Kiperete wangu…!”.
Kipindi cha nyuma wawili hawa walishakuwa katika uhusiano ya kimapenzi.
Ufafanuzi wa Jacqueline Wolper kuhusu Alikiba, ni baada ya kusema anampenda
Reviewed by Admin
on
Monday, December 04, 2017
Rating:
No comments:
DONDOSHA COMENT YAKO HAPA