Q Boy Msafi akanusha kukopi ‘Hallelujah’ ya Diamond

Msanii wa muziki Bongo, Q Boy Msafi amesema si kweli alichukua neno hallelujah kutoka kwenye ngoma ya Diamond inayokwenda kwa jina hilo pia.
Katika wimbo wa Q Boy ‘Karorero’ kuna mstari anasema, ‘hallelujah mtoto utaniua’, kitu ambacho amesema ni hali ya kutokea tu kufanana na si vinginevyo.
Hata hivyo katika mahojiano na kipindi cha The Playlist, Times Fm amesema ngoma yake hiyo ilikuwepo tangu kipindi akifanya kazi na label ya WCB inayomilikiwa na Diamond.
“So situation ile melody ya hallelujah ilikuwepo na imani kila mtu alikuwa anaijuia, baadhi ya watu ambao walikuwa kwenye rotation ya muziki ambao nilikuwa nao kabla sijautoa walikuwa wanaelewa tu kwamba hili neno hallelujah ilikuwepo tu” amesema Q Boy.
Ameongeza kuwa katika uandishi anaamini kuwa kuna vitu vinaweza kuandikwa na vikaenda kufanana na vingine lakini ieleweke si makusudi.
Q Boy Msafi akanusha kukopi ‘Hallelujah’ ya Diamond Q Boy Msafi akanusha kukopi ‘Hallelujah’ ya Diamond Reviewed by Admin on Thursday, November 16, 2017 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.