Sijawahi Kugombana na Msanii Yeyote Ila Kusema Kwangu Ukweli Ndo Kunaniponza- Baraka Da Prince



Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Barakah The Prince amesema hajawahi kugombana na msanii yeyote ila kusema kwake ukweli ndio kunafanya watu kumchukulia kama mkorofi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Sometimes’ amekiambia kipindi cha XXL, Clouds Fm kuwa baada ya kuligundua hilo ameamua kulifanyia kazi.

“Sijawahi kumtukana msanii au kugombana na msanii but ule ukweli wangu labda unamwambia mtu, unajua watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, anaweza akakuboa ukamwambia ukweli akakuchukulia tofauti kwa hiyo nadhani sana hiyo ndio ilikuwa inachangia” amesema Barakah.

“Wakati huu nimejitahidi ndio maana hata nimekaa kimya muda mrefu sana, nimejaribu kukaa na watu wengi sana wamenipa cancelling wakiwemo watu wakubwa kwenye entertainment” amesisitiza.

Pia ameongeza kuwa watu kwa sasa watamuona ni Barakah mpya kwani anajichukulia kama msanii mpya ambaye ndio anataka kutoka. 
Sijawahi Kugombana na Msanii Yeyote Ila Kusema Kwangu Ukweli Ndo Kunaniponza- Baraka Da Prince Sijawahi Kugombana na Msanii Yeyote Ila Kusema Kwangu Ukweli Ndo Kunaniponza- Baraka Da Prince Reviewed by Admin on Tuesday, November 14, 2017 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.