Kataut beki wa zamani wa Rayon Sports na mume wa muigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amefariki dunia baada ya kuugua ghafla.
Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza Kataut alikuwa mazoezini jana asubuhi.
Wakati anapoteza maisha, Kataut alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.
Mara ya mwisho, Kataut aliichezea Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.
Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.
Tanzia : Ndikumana Mume wa Irene Uwoya wa Zamani Afariki Dunia
Reviewed by Admin
on
Wednesday, November 15, 2017
Rating:
No comments:
DONDOSHA COMENT YAKO HAPA