Beki wa Kulia wa Klabu ya Simba aliyesajiliwa msimu huu kutokea Azam Shomari Kapombe amemtolea Uvivu mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba Zacharia Hanspoppe ambaye jana mapema alinukuliwa akimtaka mchezaji huyo kama anataka kubaki Simba basi aanze Kucheza.
Katika maneno ya Hanspoppe msomaji wa kwataunit.com alinukuliwa akisema Simba hawawezi kumlipa mchezaji ambaye hachezi, Hanspoppe alisisitiza kuwa Kapombe ameshapona ila anaogopa kucheza.
Shomari Kapombe amejibu.
Katika maneno ya Hanspoppe msomaji wa kwataunit.com alinukuliwa akisema Simba hawawezi kumlipa mchezaji ambaye hachezi, Hanspoppe alisisitiza kuwa Kapombe ameshapona ila anaogopa kucheza.
Shomari Kapombe amejibu.
Mimi bado nina majeraha Daktari ameniambia kama ni kucheza kwa sasa haiwezekani, labda mzunguko wa pili labda ndo naweza kucheza.
Sasa Hizo habari za kwenda kulalamika kwenye radio sizijui yeye hajaongea na mimi, kama ni suala la kuvunja mkataba wao kama wanataka kuvunja mkataba wavunje tu, mimi siogopi kucheza mimi ni mchezaji nayejielewa sana".
Shomari Kapombe ambaye aliumia wakati akiitumikia timu ya Taifa Taifa Stars akiwa kambini Stars ikijiandaa jijini Mwanza dhidi ya Rwanda aliendelea kusema.
Kama kucheza nishacheza sana , nishacheza sehemu nyingi tena kwa wakati mgumu, kwani hata kipindi kile niko Azam nilikuwa na majeruhi ila nilikuwa nacheza sijaanza kuumia niko Simba, Mimi siwezi kuogopa kucheza sababu ya Majeruhi na mimi siwezi kucheza nikiwa majeruhi na siwezi kuogopa kucheza nikiwa nimepona
Hata hivyo leo Uongozi wa Klabu ya Simba unatarajiwa kulitolea ufafanuzi zaidi suala hilo, Kaa nasi tutakujuza zaidi
SHOMARI KAPOMBE AMTOLEA UVIVU HANSPOPPE
Reviewed by Admin
on
Tuesday, November 14, 2017
Rating:
No comments:
DONDOSHA COMENT YAKO HAPA