KIATU CHA HIMID MAO, KIMEMJERUHI MKATA UMEME WA YANGA VIBAYA, KURUDI LABDA ZAIDI YA WIKI TATU


Kiungo Mzambia, Justine Zulu alilazimika kutoka nje na nafarsi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin baada ya kukumbana na kiatu cha nahodha wa Azam FC, Himid Mao.

Yanga imeitwanga Azam FC kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Awali ilionekana kama mzaha, lakini Zulu ameshonwa zaidi ya nyuzi tatu na imeelezwa huenda itachukua kuanzia wiki mbili hadi mwezi kwake kurejea tena uwanjani.

Hata hivyo, mmoja wa wauguzi waliomchukua kumtoa nje, amesema inawezekana akapona haraka.

Zulu alipiga shuti na Himid akaingiza mguu, iinaonekana kiatu ndiyo kilichomjeruhi.

Credit  By SalehJembeBlog

KIATU CHA HIMID MAO, KIMEMJERUHI MKATA UMEME WA YANGA VIBAYA, KURUDI LABDA ZAIDI YA WIKI TATU KIATU CHA HIMID MAO, KIMEMJERUHI MKATA UMEME WA YANGA VIBAYA, KURUDI LABDA ZAIDI YA WIKI TATU Reviewed by Admin on Sunday, April 02, 2017 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.