HUU NDIO UKWELI KUHUSU KESI YA MSANII MO MUSIC


Mahakama ya mjini Dodoma imefuta kesi ya utapeli iliyokuwa ikimkabili Msanii wa bongo Fleva,Mo music ambapo msanii huyo alikuwa akituhumiwa kama mtuhumiwa wa pili.
Kesi hiyo iliibuka baada ya mpenzi wa zamani wa Mo Music kumtapeli mwanaume mmoja anayesadikiwa kuwa ni mpenzi wake mpya pesa zaidi ya shilingi milioni 30 mwishoni mwa mwaka jana huko dodoma na kuaminika kuwa alimpelekea msanii huyo pesa hizo.
Mo Music amekana na kusema si kweli kwamba alicheza mchezo huo na mpenzi wake wa zamani na kuongeza kuwa mwanamke huyo amekuwa akimletea kadhia mara kwa mara hasa pale anapotaka kutoa wimbo hata kufikia hatua ya kuzusha kuwa ana ujauzito wa msanii huyo.
Source:Ayo Tv
HUU NDIO UKWELI KUHUSU KESI YA MSANII MO MUSIC HUU NDIO UKWELI KUHUSU KESI YA MSANII MO MUSIC Reviewed by Admin on Tuesday, February 23, 2016 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.