Mrembo Jokate Mwegelo akataa kujibu kuhusu Alikiba

Jokate Mwegelo amekata kuweka wazi kati yake na Alikiba nani hasa alimbwaga mwenzake katika mahusiano yao.

Katika mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio aliulizwa; ‘wewe ulimwaacha Alikiba au Alikiba alikuacha wewe’, na jibu la Mwanamitindo hiyo likawa; ‘siwezi kujibu’.
Katika hatua nyingine amezungumzia suala la kuonekana zaidi katika siasa na mipango yake ya kazi katika brand yake ya Kidoti.
“Actually tupo kwenye process ya kufanya rebrand ya kidoti kwa hiyo very soon mtaweza kushuhudi bidhaa zetu zikiingia sokoni, kuna model mbali mbali kama unakumbuka miezi kadhaa nilifanya usahili wa warembo wapya ambao tutawatumia kwenye bidha zetu pia kuna bidhaa mpya” amesema.
Mrembo Jokate Mwegelo akataa kujibu kuhusu Alikiba Mrembo Jokate Mwegelo akataa kujibu kuhusu Alikiba Reviewed by Admin on Friday, November 10, 2017 Rating: 5

No comments:

DONDOSHA COMENT YAKO HAPA

Powered by Blogger.